SLIDE SHOWS ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA WAIGIZAJI MKOA WA KINONDONI......LOL

Chama Cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni Photos Slideshow: CHAMA’s trip to Dar es Salaam, Tanzania was created by TripAdvisor. See another Dar es Salaam slideshow. Take your travel photos and make a slideshow for free.

Saturday, December 10, 2011

MATUKIO MBALIMBALI YA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA

Rais Jakaya Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania kikosi hiki ni cha Jeshi la Wananchi wanawake

Rais Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na viongozi wa nchi mbalimbali waliohudhuria katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania yanayofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam mchana huu hapa akisalimiana na Rais wa Namibia Mheshimiwa Hifikepunye Pohamba.

Rais jakaya Kikwete akipokea heshima wakati mizinga ikipigwa na jeshi la wananchi kwa heshima ya Rais.

Rais Dk. Jakaya Kikwete akipungia mkono wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja wa uhuru kwa ajili ya kuongoza sherehe za miaka 50 ya Tanzania.
Msafara wa Rais Dk Jakaya Kikwete ukiwasili kwenye uwanja wa Uhuru tayari kwa kuongoza watanzania katika sherehe za miaka 50 ya Tanzania.