TDFAA CONSTITUTION KATIBA YA CHAMA CHA WAIGIZAJI WA PICHA JONGEFU TANZANIA (TDFAA) TANZANIA DRAMA & FILM ACTORS ASSOCIATION KATIBA IMEANDALIWA NA KAMATI KAZI (TDFAA) 17/05/2011 |
g. Kutoa leseni na kitambulisho kwa kila Mwanachama ili kutambulika kuwa ni muigizaji wa picha jongefu/Filamu Tanzania.
h. Kushusha na kupandisha madaraja ya waigizaji ya waigizaji kulingana na uwezo uliotukuka, ufanisi na ubunifu..
i. Kutangaza kazi za waigizaji wa picha jongefu/Filamu walio wanachama ndani na nje ya nchi.
j. Kuklinda na kuhifadhi tamaduni za Taifa letu.
k. Kutoa adhabu kwa watakaokiuka maadili ya Nchi yetu na maadili ya taluma ya uigizaji.
l. Kumfutia leseni ya uigizaji Mwanachama aliyeshindikana kimaadili.
m. Kuandaa na kuendesha mikutano, maonyesho semina, makongamano, washa, mashindano na matamasha ya fani ya uigizaji ili kukuza na kupata waigizaji bora na vikundi bora.
n. Kufuatilia haki za Wanachama na kuwasaidia katika mikataba ya kazi zao za kisanii.
o. Kushirikiana na vyama vingine popote duniani vinavyojihusisha na maswala ya sanaa na wanii.
p. Kuanzisha na kuendeleza miradi yenye kuleta faida kwa ajili ya kuongeza kipato cha Chama.
q. Kuelimisha/kuhamasisha umma kuhusu maswala mbalimbali ya kijamii kama UKIMWI n.k.
SURA YA TATU
UANACHAMA:
i. Wanachama wa TDFA watakuwa ni:-
a. Waigizaji wote wa picha jongefu/Filamu Tanzania bara.
b. Awe amewahi kuigiza kazi yoyote ya picha jongefu japo moja.
c. Awe ni mtu anayefahamu tasnia ya uigizaji wa Picha jongefu/Filamu.
d. Awe ni mtu mwenye uwezo wa kubuni mawazo ambayo yanaweza kuboresha uigizaji wa picha jongefu/Filamu.
e. Awe mtu mwenye kuthamini maadili ya kijamii katika ubunifu wake.
f. Awe na akili timamu.
g. Awe raia wa Tanzania au raia mkazi.
ii. Mwanachama aliye nje ya Nchi kwa muda mrefu ataendelea kutambuliwa kuwa Mwanachama endapo atatoa taarifa maalumu katika /chama na atawasilisha michango yake ndani ya Chama.
iii. Wajibu wa wanachama itakuwa ni:-
a. Kulipa ada na michango yote halali iliyoidhinishwa kwa mujibu wa Katiba na vikao halali.
b. Kuhudhuria vikao vyote vitakavyoitishwa na Chama.
c. Kila Mwanachama ana wajibu wa kulipa ada ya uanachama kila mwezi na iwapo Mwanachama atapitiliza miezi mitatu bila kulipa ada atapoteza haki zake za msingi.
d. Ni wajibu wa Mwanachama kufanya kazi ya uigizaji akiwa na kitambulisho na leseni iliyo hai.
e. Kuheshimu, kuitetea na kuitekeleza Katiba.
f. Kuwa ni mwenye maadili mazuri.
g. Kuigiza kazi zenye kuelimisha, kufurahisha, kuburudisha, kuasa na kuonya jamii.
h. Awe na ari ya kujituma na kujiendeleza kitaaluma.
iv. Haki za wanachama zitakuwa ni:-
a. Wanachama wote wana haki sawa.
b. Wanachama wana haki ya kupata taarifa zote za chama kupitia ngazi husika.
c. Wanahaki za kuchagua na kuchaguliwa katika ngazi mbalimbali za uongozi.
d. Kuhudhuria mikutano ya Chama.
e. Kupiga na kupigiwa kura.
f. Kupata misaada ya hali na mali kutoka kwenye /chama kadiri itakavyowezekana.
g. Kupata taarifa ya mapato na matumizi kwa mujibu wa Katiba.
h. Kuwa na haki ya kuchukua Fomu ya kuomba uongozi na kuchaguliwa katika nafasi ya uongozi wa shirikisho la Filamu ikiwa ana sifa zinazostahili.
i. Kulindwa na kutetewa na /chama pale inapobidi.
j. Haki ya kukosoa na kukosolewa kwa kufuata taratibu za Chama.
k. Haki ya kushitaki na kushitakiwa kisheria.
l. Haki ya kuheshimu na kuheshimiwa, kuthamini na kuthaminiwa utu wake.
m. Atakuwa na haki ya kusaidiwa kisheria iwapo haki yake imekiukwa.
v. Aina za uanachama:
a. Wanachama wa Kujiunga.
Wanachama wa kujiunga ni wanachama wote wanaoigiza Filamu, Tamthiliya na michezo ya kuigiza ya jukwani wale wanaokidhi sifa zilizoainishwa katika sura tatu ya Katiba ya Chama.
b. Wanachama wa kutunukiwa:
Wanachama wa kutunukiwa ni wale wanaotunukiwa kutokana na mchango wao katika fani ya uigizaji, mkutano mkuu wa Chama ndio utakaokuwa na mamlaka ya kuidhinisha wanachama hao baada ya kupokea mapendekezo ya Bodi.
c. Uanachama wa muda:
Uanachama huu utahusisha wageni watakaoingia nchini kufanya kazi ya uigizaji. Uanachama huu utakuwa kwa muda ambao mhusika atafanya kazi hapa nchini.
vi. Taratibu za kuwa mwanachama:
a. Maombi yote yapelekwe kwa njia ya kujaza Fomu katika Bodi kwa ajili ya kujadiliwa.
b. Wanachama wanaojiunga watalipia ada ya Fomu ya kujiunga.
vii. Kukoma uanachama:
a. Kwa kujiondoa au kujiudhuru kwa hiari.
b. Kufukuzwa kutokana na kuvunja Katiba au kutotimiza masharti na kanuni za Chama baada ya kuthibitishwa na zaidi ya nusu ya Wajumbe katika mkutano Mkuu wa Chama.
c. Kifo cha Mwanachama.
d. Kutohudhuria mikutano mikuu mitatu bila ya taarifa.
e. Chama Mwanachama kuvunjwa kwa kufuata taratibu za kisheria.
f. Kupatwa na wazimu uliodhibitishwa na Daktari.
g. Mwanachama aliyekoma kuwa Mwanachama hatarudishiwa ada ya uanachama au michango yoyote aliyowahi kutoa wakati akiwa Mwanachama.
SURA YA NNE
VIKAO
Kutakuwa na aina tatu za vikao:
a. Mkutano Mkuu
b. Mkutano maalum
c. Mkutano wa dharula
i. Mkutano Mkuu Taifa
Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa chama kitaifa na chama kimkoa, Mkutano Mkuu wa chama ndiyo utakaowachagua viongozi wa chama kwa mujibu wa katiba.
a. Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Chama Kitaifa ambao utafanyika miezi mitatu kabla ya mkutano mkuu wa TAFF.
b. Mkutano maalum wa wanachama wote utafanyika mara moja kila mwaka.
c. Mkutano wa Dharula utafanyika endapo kutakua na dharula yeyote yenye haja ya kutekelezwa kwa wakati huo.
ii. Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa watakuwa ni:-
a. Mwenyekiti
b. Makamu Mwenyekiti
c. Katibu Mkuu wa chama Taifa
d. Wajumbe wa Bodi 9
e. Maafisa watendaji, wakuu wa idara za chama ambao hawatakuwa na haki ya kupiga kura.
f. Wajumbe watatu kutoka ngazi ya Mikoa yote Tanzania (Viongozi wakuu wa Chama), Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu.
g. Wajumbe wa kualikwa kwa idadi na uwakilishi utakaoamuliwa na Bodi. (wajumbe hawa hawatakuwa na haki ya kupiga kura.)
h. Muwakilishi mmoja kutoka shirikisho la Filamu, TAFF.
i. Wageni waalikwa wasiozidi watano au kadiri uongozi utavyoona inafa kwa sababu maalumu.
iii. Kazi za Mkutano Mkuu Taifa zitakuwa:-
a. Kuidhinisha kanuni na mikakati ya Chama
b. Kuchagua viongozi wa Chama ngazi ya Taifa
c. Kupokea taarifa za mapato na matumizi ya mwaka uliotangulia,
d. Kupokea, kujadili na kuidhinisha ripoti ya utendaji ya mwaka uliotangulia.
e. Kuidhinisha mipango na bajeti ya mwaka unaofuata.
f. Kuondoa kiongozi yeyote katika madaraka kutokana na makosa mbalimbali baada ya kuthibitishwa.
g. Mwenyekiti ndiye atakuwa muendeshaji wa Mkutano Mkuu.
h. Katibu Mkuu atakuwa Katibu wa mkutano huu.
i. Tarifa ya Mkutano Mkuu itatolewa angalau mwezi mmoja kabla, ikielezea tarehe, saa, mahali na ajenda za Mkutano.
j. Akidi ya Mkutano Mkuu itakuwa nusu ya wajumbe wote wenye haki ya kupiga kura.
k. Katibu ataandika kumbukumbu za mkutano na kubzihifadhi kwa matumizi ya baadae ya wanachama, wajumbe wa bodi na Menejimenti ya chama.
iv. BODI TAIFA
Kutakuwa na Bodi ambayo itakuwa na Wajumbe 13 wafuatao:-
a. Mwenyekiti
b. Makamu Mwenyeki
c. Katibu Mkuu
d. Mtunza Hazina
e. Wajumbe wengine tisa watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa uchaguzi.
f. Bodi itakuwa na uwezo wa kualika mtu yeyote kwa ajili ya kuisaidia katika kujadili jambo lolote lililo kwenye ajenda, ingawa hatakuwa na haki ya kupiga kura.
g. Mikutano ya Bodi itafanyika kila baada ya miezi mitatu, au mara nne kwa mwaka.
h. Mwenyekiti wa chama ndiye atakuwa Mwenyekiti wa vikao vyote vya Bodi.
i. Katibu Mkuu ndiye atakuwa Katibu wa Bodi na attandika kumbukumbu na kuzihifadhi kama kumbukumbu sahihi.
j. Akidi ya mikutano ya Bodi itakuwa ni nusu ya wajumbe wenye haki ya kupiga kura.
v. Kazi ya Bodi ya Taifa itakuwa ni::-
a. Kuandaa na kuhuisha sera, malengo, mikakati na miongozo mingine yoyote ya Chama.
b. Kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa shughuli na mipango ya chama.
c. Kuandaa miongozo na taratibu za fedha, utumishi na utawala.
d. Kusimamia matumizi sahihi ya rasilimali za Chama kama vile fedha, watumishi na vifaa.
e. Kuidhinisha mikataba ya Chama na watu au asasi mbalimbali za ndani na nje ya Nchi.
f. Kutafuta fedha kwa ajili ya kugharimia shughuli za Chama.
g. Kuthibitisha mipango na bajeti ya mwaka kabla ya kuwasilishwa kwenye Mkutano Mkuu.
h. Kuthibitisha ripoti za mwaka za utendaji na fedha kabla ya kuwasilisha kwenye mkutano mkuu.
i. Kuandaa ajenda za Mkutano Mkuu.
j. Kuteua wakaguzi wa mahesabu ya Chama.
k. Kuthibitisha Wanachama wanaogombea uongozi kwa ajili ya kupelekwa kwenye Mkutano mkuu kwa ajili ya uchaguzi.
l. Kusimamisha uanachama wa Wanachama wenye makosa na kupata righaa ya Mkutano Mkuu ya kufukuzwa kabisa.
m. Kusimamisha wajumbe wa bodi wanaokiuka masharti ya kazi zao na kupata ridhaa ya Mkutano Mkuu ya kuwafukuza kabisa.
n. Kuajiri watendaji mbalimbali wa Chama na maafisa wengine kadiri itakavyoona inafaa.
o. Kutekeleza maagizo mbalimbali kutoka shirikisho la Filamu, TAFF, ili kurahisisha. Utendaji wake, Bodi itakuwa na uwezo wa kuunda Kamati ndogo za kudumu au za muda kwa ajili ya shughuli maalumu.
vi. Mkutano Mkuu wa Mkoa
a. Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Chama Mkoa ambao utafanyika miezi mitatu kabla ya mkutano mkuu wa TDFAA Taifa.
b. Mkutano wa kawaida wa Wanachama wote utafanyika mara moja kila mwaka.
c. Mkutano wa Dharula utafanyika endapo kutakuwa na dharula yeyote yenye haja ya kutekelezwa kwa wakati huo.
vii. Wajumbe wa Mkutano Mkuu Mkoa watakuwa ni:-
a. Mwenyekiti
b. Makamu Mwenyekiti
c. Katibu Mkuu wa Chama Mkoa
d. Wajumbe wa Bodi 9
e. Wanachama wote wa TDFAA ngazi ya Mkoa
f. Maafisa Watendaji, wakuu wa idara za Chama ambao hawatakuwa na haki ya kupiga kura.
g. Wajumbe wa kualikwa kwa idadi na uwakilishi utakaoamuliwa na Bodi. (Wajumbe hawa hawatakuwa na haki ya kupiga kura.)
h. Muwakilishi mmoja kutoka, FDFAA Taifa.
i. Wageni waalikwa wasiozidi watano au kadiri uongozi utakavyoona inafaa kwa sababu maalumu.
viii. Kazi za Mkutano Mkuu zitakuwa:-
a. Kuidhinisha kanuni na mikakati ya Chama.
b. Kuchagua viongozi wa Chama
c. Kupokea taarifa za mapato na matumizi ya mwaka uliotangulia.
d. Kupokea, kujadili na kuidhinisha ripoti ya utendaji ya mwaka uliotangulia.
e. Kuidhinisha mipango na bajeti ya mwaka unaofuata.
f. Kuondoa kiongozi yeyote katika madaraka kutokana na makosa mbalimbali baada ya kuthibitishwa.
g. Kuidhinisha Wanachama wapya.
h. Kuidhinisha kufukuzwa kwa Wanachama.
i. Wenyekiti ndiye atakuwa muendeshaji wa Mkutano Mkuu.
j. Katibu Mkuu atakuwa Katibu wa Mkutano huo.
k. Taarifa ya Mkutano Mkuu itatolewa angalau mwezi mmoja kabla, ikielezea tarehe, saa, mahali na ajenda za Mkutano.
l. Akidi ya Mkutano Mkuu itakuwa nusu ya Wajumbe wote wenye haki ya kupiga kura.
m. Katibu ataandika kumbukumbu za Mkutano na kuzihifadhi kwa matumizi ya baadae ya Wanachama, Wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Chama.
ix. Bodi ya Mkoa
Kutakuwa na Bodi ambayo itakuwa na Wajumbe 13 wafuatao:-
a. Mwenyekiti
b. Makamu Mwenyekiti
c. Katibu Mkuu
d. Mtunza Hazina
e. Wajumbe wengine tisa watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa uchaguzi.
f. Bodi itakuwa na uwezo wa kualika mtu yeyote kwa ajili ya kuisaidia katika kujadili jambo lolote lililo kwenye ajenda, ingawa hatakuwa na haki ya kupiga kura.
g. Mikutano ya Bodi itafanyika kila baada ya miezi mitatu au mara nne kwa mwaka.
h. Mwenyekiti wa Chama ndiye atakuwa Mwenyekiti wa vikao vyote vya Bodi.
i. Katibu Mkuu ndiye atakuwa Katibu wa Bodi na attandika kumbukumbu na kuzihifadhi kama kumbukumbu sahihi.
j. Akidi ya mikutano ya Bodi itakuwa ni nusu ya Wajumbe wenye haki ya kupiga kura.
x. Kazi za Bodi itakuwa ni:-
a. Kuandaa na kuhuisha sera,, malengo, ikakati na miongozo mingine yoyote ya Chama.
b. Kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa shughuli na mipango ya chama.
c. Kuandaa miongozo na taratibu za fedha,, utumishi na utawala.
d. Kusimamia matumizi sahihi ya rasilimali za chama kama vile fedham watumishi na vifaa.
e. Kuidhinisha mikataba ya Chama na watu au asasi mbalimbali za ndani na ya Nchi.
f. Kutafuta fedha kwa ajili ya kugharimia shughuli za Chama.
g. Kuthibitisha mipango na bajeti ya mwaka kabla ya kuwasilishwa kwenye Mkutano Mkuu.
h. Kuthibitisha ripoti za mwaka za utendaji na fedha kabla ya kuwasilishwa kwenye Mkutano Mkuu.
i. Kuandaa ajenda za Mkutano Mkuu.
j. Kuteua wakaguzi wa mahesabu ya Chama.
k. Kuthibitisha Wanachama wapya kwa ajili yakuidhinishwa na Mkutano Mkuu.
l. Kuhakiki Wanachama wanaogombea uongozi kwa ajili ya kupelekwa kwenye Mkutano Mkuu kwa ajili ya uchaguzi.
m. Kusimamisha uanachama wa Wanachama wenye makosa na kupata ridhaa ya mkutano mkuu ya kuwafukuza kabisa.
n. Kuajiri watendaji mbalimbali wa chama, na maafisa wengine kadiri itakavyoona inafaa.
o. Kutekeleza maagizo mbalimbali kutoka shirikisho, TAFF,
p. Ili kurahisisha utendaji wake, Bodi itakuwa na uwezo wa kuunda Kamati ndogo za kudumu au za muda kwa ajili ya shughli maalumu.
xi. Secretarieti Taifa/Mkoa.
i. Kutakuwa na Sekreterieti ambayo itakuwa na:-
a. Katibu Mkuu ambaye atakuwa kiongozi wa Sekreterieti
b. Mweka Hazina/Mhasibu wa Chama
c. Wakuu wa Vitengo mbalimbali
d. Maafisa wengine wa Chama.
ii. Sekreterieti itakutana kadri itakavyoona inafaa na itakavyopanga.
iii. Katibu Mkuu atakuwa Mwenyekiti wa vikao vya /sekreterieti.
xii. Kazi za Sekreterieti zitakuwa:-
a. Kutekeleza maamuzi na maagizo ya Bodi
b. Kuandaa mipango ya kutafuta fedha na mitaji
c. Kujenga mashirikiano na wadau muhimu
d. Kuandaa ripoti ya mwaka ya utekelezaji wa kazi
e. Kuandaa ripoti ya mwaka ya mapato na matumizi
f. Kuandaa mpango na bajeti ya mwaka unaofuatia.
g. Kusimamia na kuhakiki mali za Chama.
SURA YA TANO:
VIONGOZI WA CHAMA
i. Mwenyekiti wa Chama
a. Atachaguliwa na Mkutano Mkuu kila baada ya miaka mitatu.
b. Atakuwa mjumbe katika Mkutano Mkuu wa shirikisho la Filamu
c. Ataweza kughaguliwa kwa vipindi viwili tu.
d. Atakuwa Msimamizi Mkuu wa shughuli zote za chama.
e. Atakuwa na kura ya veto (turufu) iwapo kura zote za Wajumbe wanaoafiki na wasioafiki zitakuwa sawa.
f. Atakuwa Mwenyekiti wa vikao vya Bodi na Mkutano Mkuu.
g. Atathibitisha matumizi ya pesa kiasi kitakachoamuliwa na Bodi kwa wakati huo.
h. Atawajibika kwenye Mkutano Mkuu.
ii. Makamu Mwenyekiti wa chama Taifa/Mkoa
a. Atachaguliwa na Mkutano Mkuu kila baada ya miaka mitatu.
b. Kuwa Makamu Mwenyekiti hakumuondelei haki ya kugombea uenyekiti hata kama Mwenyekiti aliyekuwa Makamu wake atamaliza muda wake.
c. Atakaimu majukumu ya Mwenyekiti atakapokuwa hayupo.
d. Atamshauri Mwenyekiti juu ya mambo mbalimbali ya Chama.
e. Atakuwa mjumbe wa Bodi.
f. Atafanya kazi nyingine zozote atakazopewa na Mwenyekiti na maamuzi ya vikao halali.
g. Atawajibika kwa Mwenyekiti.
iii. Katibu Mkuu Taifa / Mkoa
a. Atachaguliwa katika mkutano mkuu wa uchaguzi na atakuwa madarakani kwa miaka mitatu.
b. Ataweza kuongezewa mikataba kadiri itakavyoonekana inafaa.
c. Atakuwa mjumbe katika mkutano mkuu wa Shirikisho, TAFF.
d. Atawajibika kuitisha vikao vyote vya chama baada ya kuwasiliana na Mwenyekiti wa Chama.
e. Atakuwa Katibu wa vikao vyote vya Bodi.
f. Atabuni na kutayarisha miradi ya Chama.
g. Atafanya mawasiliano yote ya kiutendaji ya ndani na nje ya Chama.
h. Atakuwa msemaji mkuu kwenye masuala ya kiutendaji.
i. Atatunza kumbukumbu zote za Chama
j. Atakuwa Mjumbe wa Bodi ya Chama.
k. Atawajibika kwa Mwenyekiti wa Chama.
iv. Mweka Hazina wa Chama
a. Atajiriwa na Bodi kwa Mkataba wa miaka mitatu.
b. Ataweza kuongezewa mikataba kadiri itakavyoonekana inafaa.
c. Atatakiwa kuwa na angalau stashahada ya uhasibu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa kisheria.
d. Atakuwa ndiye mfuatiliaji mkuu wa mapato na matumizi ya ndani na nje ya Chama na akufanya matumizi.
e. Atahusika na uaandaaji wa malipo mbalimbali.
f. Atawajibika kukusanya ada na michango yote halali ilipotishwa na kuikatia risiti.
g. Atatoa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha katika Mkutano Mkuu na kwa bodi kila miezi mine.
h. Atahusika kuweka fedha za chama Benki.
i. Atafanya shughuli zake kwa kufuata sheria na kanuni za fedha za shirikisho pamoja na taratibu za kitaifa na kimataifa za uhasibu na utunzaji wa mahesabu.
j. Atashirikiana na wakaguzi wa Fedha wa ndani na nje ya Chama.
k. Atatoa hati za malipo yote katika shughuli za kifedha.
l. Atawajibika kwa Katibu Mkuu.
m. Kabla ya kuajiriwa, Bodi ya Chama itamteua Mjumbe mmojawapo kutoka miongoni mwa Wajumbe wa bodi kushika nafasi ya Uhasibu kwa muda mpaka atakapoajiriwa.
SURA YA SITA
Sifa za viongozi Taifa / Mkoa
Isipokuwa mahali ilipoelezwa vinginevyo, sifa na wajibu wa kiongozi itakuwa:-
1. Kuwa mwanachama wa Chama
2. Awe na umri usiopungua miaka 21 kwa nafasi nyingine za kuchaguliwa isipokuwa kw anafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti tu.
3. Kuwa na Elimu isiyopungua kidato channe au inayofanana na hiyo.
4. Kuwa raia wa Tanzania.
5. Kutokuwa na historia ya kufungwa jela.
6. Kuwa mtu mwaminifu na mwadilifu.
7. Awe na akili timamu.
8. Kufanya kazi kulingana na kanuni na taratibu zilizowekwa.
9. Kufanya kazi kwa bidii na ufanisi mkubwa.
10. Kuwa mtu anayeheshimu, kuheshimika na kuheshimu wengine.
11. Kutojihusisha na matendo ya dhuluma, rushwa au upendeleo.
12. Kuwa mwangalifu katika matumizi ya rasilimali za Chama.
13. Kujiepusha na uropokaji na utoaji wa taarifa za Chama kwa watu wa nje bila kufuata utaratibu uliowekwa.
14. Kutetea na kujenga hadhi na jina zuri la Chama.
15. Kwa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Chama asiwe chini ya umri wa miaka 30.
16. Awe Muigizaji wa Picha jongefu.
SURA YA SABA:
MASUALA YA UCHAGUZI
Mkutabo Mkuu maalumu wa uchaguzi:-
1. Utafanyika kila baada ya miaka mitatu.
2. Utakuwa na Wajumbe malum wa ziada ambao hawatakuwa na haki ya kupiga kura ila ni wasimamizi/waangalizi wa uchaguzi.
3. Mwaka wa uchaguzi utakuwa kwa wanachama wote. Kila Chama kitafanya uchaguzi mwaka huo.
4. Ratiba ya uchaguzi itaanzia katika vyama wanachama na kumalizika kwa uchaguzi katika Shirikisho la Picha jongefu/Filamu.
5. Uchaguzi utakuwa kwa kura za siri.
6. Watakaopata kura nyingi zaidi kuliko wagombea wengine watatangazwa washindi.
7. Viongozi watakaochaguliwa ni Mwenyekiti,, Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu, pamoja na wajumbe 9 wa Bodi.
8. Suala la uwiano na jinsia litazingatiwa wakati wa uchaguzi wa viongozi.
9. Bodi ya Chama itatayarisha kanuni mbalimbali za uchaguzi na wagombea wa nafasi za uongozi watahakikiwa na Bodi na kukabidhi tarifa hiyo Shirikisho la Filamu nchini, TAFF. Hata hivyo Bodi haitamzuia mtu yeyote kugombea nafasi yoyote katika Chama au shirikisho endapo ana sifa na anatimiza masharti yote na kanuni zitakazowekwa.
10. Uchaguzi unapokaribia, Bodi itaandaa kanuni na taratibu za uchaguzi na kuzitangaza kwa wanachama.
11. Kutakuwepo na uchaguzi mdogo kujaza nafasi zilizoachwa wazi kwa sababu yoyote ile.
12. Utaratibu wa kuchagua viongozi ngazi ya Mkoa hautakuwa tofauti na ule Chama ngazi ya Taifa.
13. Uchaguzi mdogo utafanywa na Mkutano Mkuu wa mwaka unaofuatia.
14. Ikiwa nafasi ya Mwenyekiti itaachwa wazi, Makamu Mwenyekiti atakaimu mpaka uchaguzi mdogo utakapofanyika.
15. Endapo nafasi ya Mwenyekiti na Makamu wake zitakuwa wazi, Bodi itamchagua mtu wa kukaimu nafasi hiyo hadi uchaguzi mdogo utakapofanywa na Mkutano Mkuu unaofuata, na iwapo nafasi ya Mwenyekiti na Makamu wake itakuwa wazi miezi sita kabla ya uchaguzi mkuu, nafasi husika haitajazwa mpaka uchaguzi mkuu ila Bodi ya Chama ichague mmoja kati ya Wajumbe wa bodi kukaimu nafasi hiyo.
16. Nafasi itakayokuwa wazi katika Bodi haitajazwa hadi uchaguzi mdogo utakapofanyika. Pale ambapo idadi ya Wajumbe inayobaki ni chini ya watano, Bodi itachagua idadi inayopungua kwenye watano ili kukaimu ujumbe wa Bodi hadi uchaguzi mdogo utakapofanyika.
17. Viongozi wote wa kuchaguliwa watajiuzulu nafasi zao siku thelathini kabla ya uchaguzi Mkuu na Msemaki katika kipindi hicho atakuwa Katibu Mkuu akisaidiwa na Afisa wa habari na uhusiano wa Chama na Sekreterieti itaendelea na majukumu yake kama kawaida.
18. Uchaguzi Mkuu wa Chama ngazi ya Taifa utasimamiwa na Shirikisho la Picha jongefu/filamu nchini na uchaguzi wa Chama ngazi ya Mkoa utasimamiwa na Chama ngazi ya Taifa kuanzia kupitia fomu za maombi, kuchuja wagomea, kuwajadili na kuidhinisha majina ya wagombea kwa nafasi zao na kuzitangaza kwa wadau kupitia vyombo mbalimbali vya habari na pia kutangaza siku na tarehe ya uchaguzi.
19. Chaguzi zote kuu za tasnia ya Filamu/Picha jongefu zitafannyika mwaka mmoja ikianzia katika vyama ngazi ya Mkoa, Taifa mpaka katika Shirikisho.
20. Endapo Mwanachama aliye kiongozi atathibitika kuwa na hatia ya kosa la jinai na kuhukumiwa kifungo kwa mujibu wa sheria atakoma uongozi.
21. Kiongozi akituhumiwa kosa la jinai na kesi kuwa katika upelelezi, akiwa nje kwa dhamana atasimama uongozi, endapo akithibitika kuwa hana hatia atarudi katika uongozi kwa nafasi aliyotumikia.
SURA YA NANE
MAPATO YA TDFAA
Mapato ya TDFAA yatatokana na vyanzo vifuatavyo:-
i. Ada na michango ya wanachama itakayowekwa na bodi na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu.
ii. Makato na michango mbalimbali inayotokana na wanachama wake au wadau mbalimbali wa tansia ya Picha jongefu/filamu.
iii. Misaada kutoka watu na asasi mbalimbali ndani na nje ya Nchi.
iv. Kamisheni na malipo mengineyo yatakayolipwa kwa Chama kutokana na huduma itakazotoa au kazi zitakazofanywa kwa mujibu w taratibu na kanuni zitakazowekwa.
v. Riba za Benki.
vi. Shughuli za utunishaji mfuko wa Chama (fundraising).
vii Kuwa na miradi inayojitegemea ndani ya Chama.
viii Malipo ya faini kwa Wanachama wake kutokana na adhabu mbalimbali.
SURA YA TISA
SHUGHULI ZA FEDHA TAIFA / MKOA
i. Bodi itahakikisha kuwa vitabu na kumbukumbu za fedha zinatunzwa ipasavyo.
ii. Bodi itatengeneza kanuni za fedha kwa ajili ya shughuli za fedha kwa kuzingatia sheria za Nchi na taratibu nzuri za fedha za Kitaifa na Kimataifa.
iii. Fedha za Chama zitahifadhiwa katika Benki itakayochaguliwa na Bodi.
iv. Fedha itatolewa Benki kwa hundi ikiwa imewekwa saini za wale watakaoteuliwa na Bodi kwa utaratibu wa jumla au maalumu.
SURA YA KUMI
UKAGUZI WA MAHESABU YA FEDHA TAIFA / MKOA
i. Bodi itateuwa wakaguzi wa mahesabu wan je kwa ajili ya kukagua mahesabu ya Chama kwa utaratibu na masharti yatakayoainishwa na Bodi yenyewe.
ii. Mahesabu yaliyokaguliwa yataidhinishwa na Bodi na kuwasilishwa kwenye Mkutano Mkuu.
SURA YA KUMI NA MOJA
MWAKA WA FEDHA NA KAZI ZA CHAMA
1. Mwaka wa fedha na shughuli za Chama utakuwa ni mwaka wa Kalenda wa kawaida, yaani tarehe 1 Januari mpaka tarehe 31 Desemba.
2. Endapo Chama kitaanza shughuli zake katika mwezi wa mbele baada ya Januari, bado shughuli za Chama kwa mwaka huo zitaishia Tarehe 31 Desemba.
SURA YA KUMI NA MBILI
MAREKEBISHO YA KATIBA TAIFA / MKOA
1. Katiba inaweza kufanyiwa marekebisho kwa maamuzi yatakayo pitishwa na Mkutano Mkuu kwa kura ya theluthi mbili ya Wajumbe wenye haki ya kupiga kura waliohufhuria.
SURA YA KUMI NA TATU
KUVUNJWA KWA CHAMA
1. Chama cha Waigizaji nchini kinaweza kuvunjwa iwapo kuna sababu zenye ulazima kufanya hivyo.
2. Taarifa za kuvunjwa kwa Chama ziwafikie Wanachama siku 60 kabla ya Mkutano huo maalumu.
3. Iwapo wanachama wameafiki uamuzi huo, watalazimika kila mmoja kuthibitisha uamuzi huo kwa maandishi na kuyawasilisha kwa Katibu Mkuu siku 30 kabla ya Mkutano wa kwanza wa kujadili azimio la kuvunjwa kwa Chama.
4. Mikutano ya azimio la kuvunja Chama hiki itafanyika mara tatu ili kuhakikisha na kuthibitisha uamuzi huo.
5. Mkutano wa mwisho wa kufikia tamati ya Chama, uamuzi utatolewa mbele ya Shirikisho la Picha jongefu/filamu, TAFF na BASATA.
6. Chama kinaweza kuvunjwa kwa azimio la Mkutano Mkuu maalumu kwa kura ya theluthi mbili ya Wanachama wote.
7. Iwapo Chama kitavunjwa, mali zake zitapelwa shirikisho au zitagawiwa asasi zisizokuwa za biashara zenye malengo yanayofanana nay a Chama hiki au Shirikisho na baada ya asasi hizo kubainishwa na Bodi, BASATA itasimamia ugawaji huo.
8. Chama kitateuwa mwanasheria ambaye atalishauri kila haja itakapoonekana. Mwanasheria huyo atashughulikia usuluhishi kati ya Chama na mtu, watu au asasi yoyote. Atasimamia ufilisi wa Chama iwapo haja ya kufanya hivyo itajitokeza.
9. Migogoro kati ya Chama na watu weingine itakayoshindikana kumalizwa kwa njia ya usuluhishi, itapelekwa Shirikisho la Filamu, TAFF au BASATA na itaamuliwa kwa mujibu wa sheria za Nchi.
Katiba ya Chama Waigizaji wa Picha Jongefu Tanzania, imetayarishwa na
Kamati kazi TDFAA (Tanzania Drama & Film Actors Association )
©2011