1. UTANGULIZI CHAMA KIMEPANGA:-
a. Kufanya uchaguzi wa viongozi wake mwaka 2011. Huu utakuwa uchaguzi wa kwanza wa kikatiba.
b. Viongozi watakao chaguliwa watakuwa madarakani kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu (3)
c. Viongozi watakao chagliwa watakuwa ni :-
i. Mwenyekiti
ii. Makamu mwenyekiti
iii. Wajumbe tisa (9) wa bodi
d. Chama kitasambaza kanuni hizi kwa wanachama ili waweze kupitia na kuzielewa mapema na kikamilifu kwa wanachama wenye nia ya kugombea.
2. UFAFANUZI WA MATUMIZI YA MANENO:-
Katika kanuni hizi maneno yafuatayo yatatumika kwa maana inayofafanuliwa hapa chini :-
BARAZA:- Baraza maana yake ni baraza la sanaa la Taifa
BODI : - Maana yake ni bodi ya chama Taifa / Mkoa inayoundwa kwa
mujibu wa kifungu 4 cha katiba.
KATIBA :- Maana yake ni katibu mtendaji wa chama taifa mkoa aliyeanishwa katika kifungu 3 cha katiba.
MKUTANO MKUU: - Maana yake ni mkutano mkuu wa chama
MHASIBU: - Maana yake ni mweka hazina wa chama aliyeainishwa katika
kifungu cha 4 cha katiba
MWENYEKITI:-Maana yake ni mwenyekiti wa chama anayechaguliwa kwa
mujibu wa kifungu 1 cha katiba
SEKRETARIETI: - Maana yake ni sekretarieti ya chama
CHAMA: - Maana yake ni chama cha waigizaji wa picha jongefu.
UCHAGUZI TAIFA:-
3. WAJUMBE WA MKUTANO WA UCHAGUZI TAIFA NI:-
a) Wajumbe wa mkutano mkuu wa chama ambao ni :-
i. Mwenyekiti Taifa
ii. Makamu Mwenyekiti Taifa
iii. Katibu mkuu wa chama Taifa
iv. Mweka hazina wa chama Taifa
v. Wajumbe tisa (9) wa bodi ya Taifa
vi. Wawakilishi watatu kutoka kila ngazi ya mkoa ambao ni mwenyekiti , Makamu Mwenyekiti na Katibu mkuu.
b) Chama Taifa kwa ridha na kwa kushirikiana na msimamizi,kinaweza kualika watu wengi kuwa waangalizi (Observers) wa shughuli za uchafu. Hawatakuwa na haki ya kupiga kura.
MSIMAMIZI TAIFA.
Shirikisho la filamu Tanzania ndiyo Msimamizi wa uchaguzi wa Viongozi Taifa.
Wagombea wote watachukua fomu na kuzirudisha kwa mujibu wa taratibu zitakazowekwa kwa katibu mkuu chama taifa , naye atakabidhi fomu hizo kwa tume ya uchaguzi kwa utekelezaji zaidi.
UCHAGUZI WA CHAMA MKOA
WAJUMBE WA MKUTANO WA UCHAGUZI MKOA:-
1) Mwenyekiti Mkoa
2) Makamu Mwenyekiti
3) Katibu
4) Mweka hazina
5) Wajumbe 9 wa bodi
6) Wanachama hai wa chama ngazi ya Mkoa
7) Chama mkoa kinaweza kualika watu wengine kuwa waangalizi wa uchaguzi hawatakuwa na haki ya kupiga kura.
4. MSIMAMIZI MKOA.
Bodi ya chama Taifa ndiyo wasimamizi wa uchaguzi wa Mkoa.
Wagombea wote watachukua fomu na kurudisha kwa katibu mkuu wa chama mkoa naye atakabidhi kwa tume ya uchaguzi kwa utekelezaji zaidi.
c) Kazi za msimamizi zitakuwa :-
i. Kupokea fomu zilizojazwa na wagombea kutoka kwa katibu mkuu wa Taifa / Mkoa.
ii. Kupitia na kuthibitisha wagombea waliojaza fomu za uongozi baada ya bodi ya chama kuhakiki fomu hizo.
iii. Kusaili wagombea
iv. Kupitisha wagombea waliokidhi vigezo
v. Kupokea, kutafakari na kuamua rufaa za wagombea ambao majina yao yalipata pingamizi kutoka kwa wanachama dhidi ya wagombea waliopitishwa
vi. Kutangaza wagombea
vii. Kusimamia zoezi la uchaguzi
viii. Kutangaza washindi
Tume ya uchaguzi haitakuwa na haki ya kumzuia mgombea yeyote aliyekidhi vigezo na mashariti ya kugombea kwa mujibu wa katiba ya chama na kanuni zake za uchaguzi.
5. UTEUZI WAGOMBEA:-
Wagombea wote watachukua fomu na kuzirudisha kwa katibu mkuu wa chama naye atakabidhi fomu hizo kwa msimamizi wa uchaguzi kwa utekelezaji zaidi. Fomu za nafasi ya uongozi zitalipiwa kwa gharama tofauti kulingana na nafasi ya mgombea.
i. Wale wote wanaotaka kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa chama watalazimika kujaza fomu ya maelezo binafsi.
ii. Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti na makamu wa mwenyekiti wa chama lazima waugwe mkono na wanachama hai wasiopungua kumi (10) kutoka mikoa isipungua miwili (2).
iii. Wagombea wa ujumbe wa bodi lazima waugwe mkono na wanachama hai wasiopungua watano (5)
iv. Mtu anaweza kugombea nafasi zaidi ya moja / ataruhusiwa kugombea nafasi zaidi ya moja kwa kila ngaza ya chama Taifa /Mkoa.
v. Mgombea atachaguliwa kwa nafasi moja (1) tu.
vi. Mgombea lazima awe ametimiza siku tisini (90) za wanachama wake katika chama anachotoka kabla ya siku ya uchaguzi mkuu.
vii. Bodi itakuwa na haki ya kumzuia mgombea yoyote asiyekuwa na sifa na ambaye hakutimiza mashariti ya uchaguzi kwa mujibu wa katiba na kanuni.
6. SIFA ZA WAGOMBEA :-
Wagombea wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo.
i. Kuwa mwanachama hai wa chama na awe ametimiza siku tisini za uanachama wake katika chama anachotoka kabla ya siku ya uchaguzi mkuu.
ii. Awe mwigizaji wa picha jongefu
iii. Kila mgombea atarudisha fomu iliyojazwa kikamilifu pamoja na viambatanisho muhimu.
iv. Awe mtetezi wa kweli na mpigania haki za wanachama wa chama cha waigizaji.
v. Kuwa na elimu isiyopungua kidato cha nne au inayofanana na hiyo.
vi. Kuwa na umri usiopungua miaka ishirini na moja (21) kwa nafasi za wajumbe wa bodi na kwa nafasi za mwenyekiti na makamu mwenyekiti awe na umri usio pungua miaka thelathini (30)
vii. Kuwa raia wa Tanzania wa kuzaliwa.
viii. Kutokuwa na histora ya kufungwa jela
ix. Kuwa mtu mwaminifu na mwadilifu , kuwa mtu anayejiheshimu, kuheshimika na kuheshimu wengine.
x. Kutojihusisha na matendo ya rushwa au upendeleo kuwa mwangalifu katika matumizi ya rasilimali za chama cha waigizaji .
xi. Kujiepusha na uropokaji na utoaji wa taarifa za chama kwa watu wa nje bila kufuata utaratibu uliowekwa.
xii. Kutetea na kujenga hadhi na jina zuri la chama cha waigizaji.
WAJIBU WA VIONGOZI:-
1. Msimamizi atatangaza tarehe, saa mahali patakapofanyika uchaguzi mkuu.
2. Katibu mkuu atatangaza tarehe za kuchukua fomu kwa wanaotaka kugombea na tarehe ya kurudisha fomu.
3. Mara baada ya fomu kurudishwa kwa katibu mkuu bodi itazipitia fomu hizo na baada ya kuhakiki sifa na masharti yaliyowekwa zitakabidhiwa kwa msimamizi atahakiki maelezo ya wagombea katika fomu hizo.
4. Msimamizi atapanga tarehe saa na mahali kwa ajili ya kuwasaili wagombea.
5. Katibu mkuu wa chama Taifa / Mkoa ikishirikiana na Taifa / Chama Taifa wataunda kamati maalumu kwa ajili ya kuwasaili wagombea, wajumbe wa kamati hii watakuwa watu waadilifu na makini.
6. Msimamizi atatangaza majina ya wagombea waliopitishwa siku tano (5) kablaya siku ya uchaguzi.
7. Wajumbe wa mkutano wa uchaguzi wanahaki ya kupinga mgombea yeyote na kuwasilisha pingamizi hilo kwa maandishi kwa katibu lakini lazima pingamizi hilo lithibitishwe na chama anachotoka anayeweka pingamizi.
8. Wagombea walioondolewa kwenye kugombea watakuwa na haki ya kulalamika kwa msimamizi katika muda usiozidi saa arobaini na nane (48) tangu kutangazwa majina ya wagombea.
9. Endapo msimamizi ataona haja ya kutumia muda mrefu zaidi wa kuchunguza mashauri ya malalamiko na pingamizi zitakazoletwa kwake, atafanya hivyo bila kuathiri tarehe ya uchaguzi iliyopangwa.
7. KAMPENI:-
Kutakuwa na kampeni kwa wagombea siku kadhaa kabla ya uchaguzi kadri kamati itakavyoamua.
i. Siku ya uchaguzi na kabla ya upigaji kura,wagombea watapewa muda usiozidi dakika tano(5) kutoa maelezo yao binafsi na kuomba kura za wajumbe kwa nafasi wanazogombea.
ii. Maelezo ya wagombea kuwakashifu wagombea wenzao hayataruhusiwa.
iii. Wajumbe wataruhusiwa kuwauliza maswali yasiyozidi mawili (2) kwa kila mgombea .
iv. Wagombea watatoa maelezo yao na kujibu maswali ya wajumbe kwa zamu. Wagombea wengine katika nafasi ile ile watakuwa nje ya ukumbi mpaka zamu yao ya kujieleza itakapofika.
v. Wagombea wanahaki ya kufanya kampeni kwa staili yoyote wanayoona inafaa katika kuomba fursa kwa wapiga kura ili mradi isivunjwe sheria.
8. UPIGAJI KURA
a. Upigaji kura utafanyika mara baada ya wagombea kujieleza kujibu maswali ya wajumbe
b. Utaratibu wa upigaji kura utaandaliwa mapema kati ya katibu mkuu wa chama na wasimamizi wa uchaguzi katibu mkuu atatangaza utaratibu kwa wanachama.
c. Upigaji kura utakuwa wa siri.
d. Msimamizi atateuwa watu wa kumsaidia kusimamia upigaji kura na kuheshimu kura.
e. Kura zitapigwa kwa kila nafasi kwa wakati wake
f. Kutakuwa na masanduku maalum kwa ajili ya wapiga kuweka karatasi zao za kura.
g. Wagombea ambao ni wajumbe wa mkutano wa uchaguzi watashiriki katika kupiga kura
h. Idadi ya kura isizidi idadi ya wapiga kura.
9. KUHESABU KURA:-
i. Kura zilizopigwa zitahesabiwa katika chumba tofauti na kile kilichotumika kupiga kura.
ii. Kila mgombea atakuwa na haki ya kuteua wawakilishi kutoka miongoni mwa wajumbe wa Mkutano ili kumuwakilisha katika kushuhudia shughuli ya kuhesabu na kujulisha kura
iii. Masanduku yenye kura yatafunguliwa mbele ya wasimamizi na wawakilishi wa wagombea
iv. Shughuli ya kuhesabu kura itafanyika kwa uwazi mbele ya wawakilishi wa wagombea.
v. Shughuli ya kuhesabu kura ikikamilika, kura za kila mgombea zitajumlishwa , idadi ya kura za kila mmoja itaandaliwa orodha na atakabidhiwa msimamizi kwa ajili ya kutangaza mshindi au washindi.
vi. Endapo kura za wagombea kadhaa zitafungana kwa idadi kwa ajili ya nafasi moja, itabidi upigaji kura kwa nafasi hiyo urudiwe.
vii. Wagombea watakaoshiriki katika kura za marudio ni wale tu waliopata kura sawa.
10. KUTANGAZA MATOKEO:-
a. Watakaopata kura nyingi zaidi kuliko wagombea wengine wa nafasi zao watakuwa wameshinda.
b. Msimamizi atatangaza washindi wa nafasi zote baada ya upigaji kura kukamilika.
c. Msimamizi atatangaza washindi litafanyika mbele ya wajumbe.
11. RUFAA:-
Wagombea walioshindwa wataruhusiwa kukata rufaa ndani ya muda usiopungua saa 48 baada ya uchaguzi.
12. GHARAMA ZA FOMU ZA WAGOMBEA:-
WAGOMBEA TAIFA
Mwenyekiti Taifa T.Shs.50,000/=
Makamu m/kiti taifa “ 40,000/=
Wajumbe wa bodi taifa “ 20,000/=
WAGOMBEA MKOA
Mwenyekiti T.Shs.40,000/=
Makamu Mwenyekiti 30,000/=
Wajumbe wa bodi Mkoa 15,000/=.