SLIDE SHOWS ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA WAIGIZAJI MKOA WA KINONDONI......LOL

Chama Cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni Photos Slideshow: CHAMA’s trip to Dar es Salaam, Tanzania was created by TripAdvisor. See another Dar es Salaam slideshow. Take your travel photos and make a slideshow for free.

Wednesday, November 30, 2011

MSIBA NA MAZISHI YA MAREHEMU MZEE MLELA ''BABA MZAZI WA MSANII MWENZETU,YUSUPH MLELA.YALOFANYIKA LEO TAREHE 30/11/2011 PALE MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM

Kutoka kulia ni Mchekeshaji Steve Nyerere,Ally Baucha-Mwenyekiti wa Chama cha waigizaji mkoa wa Kinondoni na Makamu mwenyekiti wa Chama cha waigizaji mkoa wa Kinondoni.Muite Salum Chilwa
Muigizaji Hemedi Suleimani aloweka nywele dawa akimpa Pole Muigizaji mwenzie Yusuph Mlela kwa kufiwa na baba yake mzazi
Mzee Chilo au Ahmed Olutu akimpa pole Yusuph Mlela
JB akimpa pole Yusuph Mlela

Wasanii wakipita katika foleni kuwapatia pole wafiwa.Mbele ni Muigizaji Cathy
Hashim Kambi nae alihudhuria msiba
Wafiwa katika majonzi
Yusuph Mlela na wadogo zake wakiweka mauwa juu ya Kaburi la marehemu baba yao
Mfiwa akiweka mauwa katika kaburi la marehemu
Marehemu Mzee Geofrey Mlela enzi za uhai wake
Muumini wa Dini akisema na wafiwa
Kutoka kulia ni Producer Nice P,Hartman Mbilinyi,Ally Baucha na Salum Chilwa
Ally Baucha akisalimiana na Muigizaji Dude

MUIGIZAJI ''YUSUPH MLELA'' AFIWA NA BABA YAKE MAZAZI

Chama cha Waigizaji mkoa wa Kinondoni kinapenda kutoa salamu zake za rambirambi kwa familia ya Marehemu mzee Mlela kwa kuondokewa na Baba yao mzazi.Chama cha waigizaji kinatoa pole kwa msanii mwenzao ''Yusuph Mlela'' kwa kuondokewa na Baba yake mzazi.Mazishi yanafanyika saa kumi kamili katika makaburi ya kinondoni jijini Dar es Salaam
Inallilahi,wainalilaihi,rajiuuuni

Tuesday, November 29, 2011

SAFARI YA UCHAGUZI WA CHAMA CHA WAIGIZAJI MKOA WA MWANZA....

 viongozi wa chama cha waigizaji taifa wakisubiri bus kwa safari ya mwanza...
safari ya kwenda mwanza kusimamia uchaguzi wa mkoa wa mwanza..
mwenyekiti wa mkoa wa ilala na mjumbe wa taifa wa chama cha waigizaji husna mgeni akiwa na mjumbe wa taifa wilson ishengoma wakiwa wanapata chakula katiakati ya safari yao ya mwanza..
Wanachama wa chama cha waigizaji mkoa wa mwanza walivyojumuika kupiga kura
Wagombea wa ujumbe wa chama cha waigizaji mkoa wa Mwanza
Mwenyekiti wa chama cha waigizaji taifa (Mike Sangu) akiwa na makamu wake Ramadhani Kingalu (kulia) pamoja na mwenyekiti wa chama cha waigizaji mkoa wa Ilala (Husna Mgeni) wakitoa maelekezo kabla ya kupiga kura.
Mwanachama wa chama cha waigizaji mkoa wa Mwanza akiuliza swali kwa mgombea ujumbe
Mgombea wa ujumbe(Bw.Hassan) akijibu swali la mwanachama kabla ya kupiga kura.
Mwanachama akipiga kura
Mshindi wa Uenyekiti wa chama cha waigizaji mkoa wa Mwanza,muite Bi Anitha
Mwenyekiti wa chama cha waigizaji mkoa wa Mwanza Bi Anitha (kushoto) akiwa na Muweka Hazina Bi Chikopa (kulia)

Sunday, November 27, 2011

BAUCHA INC YAANZA KUSHOOT "RASCAT"...

 salome akiwa katika action ya mauaji alipopigwa mapanga...
 cameraman akiwashoot k-one na therapia ndani ya tamthilia ya rascat..
 Jorvinar akiwa ndani ya scene mojawapo ya rascat
 Baucha inc katika moja scene ya tamthilia mpya....
 Kay mmoja wa wasanii watakaokuwemo ndani ya tamthilia ya rascat..
 sele akiwa na dommy wakiwa wanapeana madawa ya kulevya hotelini..
mafia jorvinar akimtishia kumuua doller ndani ya tamthilia ya rascat..

Thursday, November 24, 2011

SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA WATOA CHANGAMOTO KWA MASHIRIKISHO MENGINE...

Gari la  shirikisho la muziki Tanzania. 
Ndugu Viongozi??? na sisi gari letu ni lini?? na liwe bora na zaidi ya hili.... (Hili swali tunamuuliza ndugu Simon Mwakifamba-Raisi wa shirikisho la Filamu Tanzania )

HARAMBEE YA SAJUKI YAFANYIKA...LEO

 baadhi ya wasanii,wadau na mashabiki mbali mbali waliojitokeza kuchangia swala la sajuki.

 mwenyekiti wa chama cha waigizaji mkoa wa kinondoni ali baucha akiwa na monalisa na h.baba wakisubiri kuanza kwa harambee.
 oscar nyerere na cloud na dinno wakiwa makini kwenye mkutano wa harambee ulioamuliwa kufanyika mambo matatu kila kikundi kuchangia laki moja mikoa yote minne pili ifanyinge filamu moja ya wasanii,wadau,wamiliki wa production, wasambazaji kujitolea kuifanya hiyo filamu.
 bi mwenda baada ya kuchangia mchango wake na pia ameamoleua kujitolea kucheza kwenye filamu hiyo bure.
a

 h.baba ndio alietoa wazo la kutengenezwa filamu hiyo na ni mmoja wa kujitolea kuicheza filamu hiyo.
 kiongozi wa kikundi cha jakaya arts group akitoa mchango wake....


Wednesday, November 23, 2011

MIKOA MINNE (4) YA CHAMA CHA WAIGIZAJI KUKUTANA PAMOJA KESHO TAREHE 24 NOVEMBER 2011 KUFANYA HARAMBEE YA KUMCHANGIA MWANACHAMA/MUIGIZAJI MWENZAO ''SAJUKI KILOWOKO'' AMBAE HALI YAKE KIAFYA SI NZURI

Kesho alhamisi ya tarehe 24 mwezi huu wa kumi na moja pale ukumbi wa ''Vijana Social Hall'' maeneo ya Kinondoni Vijana-studio/njia ya kwenda mwananyamala kutakuwa na harambee ya wanachama wote wa chama cha waigizaji kutoka mikoa minne ambayo ni Kinondoni,Ilala,Pwani na Temeke kumchangia mwanachama mwenzao Bw.Sajuki Kilowoko mwenye picha hapo juu.Harambee hiyo itaanza saa tisa mchana alasiri.Wanachama wote,Mashabiki wote na marafiki wote tafadhali bila kukosa,mjitokeze kuja kumchangia mwenzetu ambaye anasumbuliwa na uvimbe tumboni,gharama zake zina-cost laki mbili kwa siku na inatakiwa matibabu yake yafanyike ndani ya mwezi mzima.....Wapenda sanaa wote,wanamuziki pia msikose.Kwa anayetaka kutoa mchango na kwa bahati mbaya hatoweza kufika tafadhali anaweza kuwasilisha mchango wake,tuma kwenye akaunti namba AKIBA.C. BANK,WASTARA JUMA ISSA ACCOUNT NO:050000003047.au piga simu kwa maelezo zaidi kwa Mwenyekiti wa chama cha waigizaji mkoa wa Kinondoni 0715 994 995 au mwenyekiti wa Taifa kwa namba hizi 0718 95 13 55.
**********************************************
''SAJUKI LEO,WEWE KESHO-TUMSAIDIE''
Asanteni!!!!!

ZIARA ZAENDELEA ZA VIKUNDI KINONDONI...

wasanii wa kikundi cha nderemo.
 kikundi cha nderemo na uongozi wa mkoa kinondoni
 kikundi cha jakaya arts wakiwa na uongozi wa kinondoni.
kikundi cha wangeuye arts group wakiwa na viongozi wa kinondoni.

Tuesday, November 22, 2011

HARAKATI ZA UCHAGUZI SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA (TAFF)

tume huru ya kusimamia uchaguzi wa shirikisho la filamu wakiwafanyia usaili wagombea 14 wa uchaguzi unaotarajia kufanyia tarehe 22 dec 2011.
mgombea wa urais wa shirikisho la filamu saimon mwakifamba akiwa kwenye usaili uliofanyika basata kujiandaa na uchaguzi december 22.
 mgombea wamakamu wa rais wa shirikisho la filamu.

  
  mgombea wamakamu wa rais wa shirikisho la filamu.
mgombea ujumbe wa body ya shirikisho la filamu tanzania(TAFF)
 mgombea ujumbe wa body ya shirikisho la filamu tanzania(TAFF)
 mgombea ujumbe wa body ya shirikisho la filamu tanzania(TAFF)
mgombea ujumbe wa body ya shirikisho la filamu tanzania(TAFF)