SLIDE SHOWS ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA WAIGIZAJI MKOA WA KINONDONI......LOL

Chama Cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni Photos Slideshow: CHAMA’s trip to Dar es Salaam, Tanzania was created by TripAdvisor. See another Dar es Salaam slideshow. Take your travel photos and make a slideshow for free.

Thursday, December 8, 2011

SHERIA NA KANUNI ZA TASNIA YA FILAMU TANZANIA..


HOTUBA YA MGENI RASMI - KAIMU KATIBU MKUU BIBI SIHABA NKINGA KATIKA UFUNGUZI WA KIKAO CHA WADAU WA FILAMU KUHUSU MJADALA WA MUSTAKABALI WA TASNIA YA FILAMU KATIKA KUSHEREKEA MIAKA 50 YA UHURU NA NINI MKAKATI KATIKA MIAKA 50 IJAYO. TAREHE 07/11/2011- KATIKA UKUMBI WA VIJANA SOCIAL- KINONDONI
Ndugu viongozi na Watendaji wa Wizara
Ndugu viongozi na watendaji wa Bodi ya Filamu
Ndugu viongozi wa Shirikisho la Filamu na wanachama
Ndugu wadau wa filamu
Ndugu wanahabari
Mabibi na mabwana
Awali ya yote napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kutupa uhai na kutuwezesha kukutana hapa.  Aidha natoa shukrani nyingi kwa kunialika kuwa mgeni katika mjadala huu muhimu ukiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru. Wizara yetu imefarijika sana na jambo hili.
Ndugu washiriki,
Katika mjadala huu nimeelezwa kuwa mtapata fursa ya kuona filamu za zamani na kupitishwa katika mada tatu ambazo ni :- Hali ya Tasnia ya Filamu kabla ya uhuru mpaka sasa, Nini wajibu wa wadau wa filamu katika mstakabali wa kukua kwa tasnia ya filamu nchini na Mapitio ya Sheria na Kanuni za Filamu
Ndugu washiriki,
Ni imani yangu mtajadili kwa kina kuhusu tasnia ya filamu na mtafikia mahali pa kupata dira ya nini tufanye katika miaka 50 ijayo. Aidha ninasihi katika majadiliano yenu mzingatie namna ya kuondokana na changamoto kadhaa ambazo zimekuwa kero kwa jamii. Changamoto hizo ni pamoja na :-
·         Uwepo wa filamu nyingi zisizo na maadili,
·         ukiukwaji wa Sheria ikiwemo wakati wa utengenezaji, uonyeshwaji, usambazaji
            uingizaji holela wa filamu za nje na wasanii;
kuibuka kwa utitiri wa vibanda visivyo rasmi vinavyoonyesha filamu/video,
·         uharamia wa kazi za wasanii wa filamu.
·         filamu nyingi zinazotengenezwa kukosa weledi na kutoendana na utamaduni wa nchi, kutotangaza Utaifa, mandhari na fursa zilizopo kwa utambulisho wa taifa letu na lugha yetu ya Kiswahili na
·         wafanyakazi katika tasnia ya filamu kutopata mapato stahiki yatokanayo na jasho lao na pia Serikali kutopata maduhuli stahili yatokanayo na filamu.

Ndugu washiriki,
Mambo niliyotaja juu yapo ndani ya uwezo wenu kwani miongoni mwenu wapo watayarishaji, wasambazaji, waingizaji filamu kutoka nje, waandishi wa miswada waonyeshaji, waendeshaji wa maeneo ya maonyesho, waongozaji na waigizaji nk. Ni
matarajio ya Seriakali kwamba kila mmoja akijitambua na kutimiza wajibu wake tutaondokana na changamoto nilizozitaja juu. Aidha ninawasihi sana kufuata Taratibu, Kanuni, na Sheria nina hakika Mwanasheria wetu wa Wizara atawapitisha kwa kina.

Ndugu washiriki,
Katika nchi za wenzetu tasnia ya filamu inatoa ajira na pate kubwa kwa wasanii na pia katika uchumi wa nchi, hali ni tofauti hapa kwetu, umefika wakati sasa kwa wasanii kutoendelea kuwa na hali duni na watu wachache kufaidi jasho lao. Ongezeni ushirikiano na imarisheni umoja miongoni mwenu. Ninatambua kuwa mna vyama tisa na vyama hivyo ni wanachama wa Shirikisho la Filamu. Nia ya Serikali katika kuruhusu uanzishwaji wa vyombo hivyo ni ili kuwe na kiungo kati yenu na Serikali. Na Serikali kupitia wizara yetu imekuwa ikiwapa ushirikiano wa hali ya juu. Sina mashaka pia nao watapata fursa ya kuzungumzia umuhimu wa umoja wenu katika kusherekea miaka 50 ya Uhuru.
Ndugu washiriki,
Katika malengo ya miaka 50 ijayo; Ni matumaini ya wizara kwamba mtatengeneza filamu zenye ubunifu wa hali ya juu, weledi na viwango bila kuathiri maadili na utamaduni wetu ; ili ziweze kuingia katika soko la ushindani. Aidha hakikisheni filamu zenu zinapitia katika mamlaka inayosimamia tasnia ya filamu kabla ya utengenezaji, usambazaji, uuzaji na uonyeshaji kama sheria inavyotutaka. Kwa wale wanoapeleka filamu nje au kushiriki katika matamsha mbalimbali ijulisheni Wizara ili mpate baraka za kuipeperusha bendera yetu kwani huko mnakwenda kuitangaza nchi.
Mwisho natoa rai kwa wale wote ambao filamu zao bade hazijasilishwa kwa ukaguzi wala miswada yao kupitishwa na Bodi ya Filamu wakumbuke muda waliopewa na Serikali wa kuwasilisha kwa hiari ni miezi mitatu kuanzia tarehe 13/10/2011. Kwa kuwa walengwa ni ninyi natumia fursa hii kuwakumbusheni.
Nawatakia mjadala mwema ni mani yangu utakuwa na tija kwa tasnia ya filamu na Taifa kwa ujumla.
Tumethubutu, Tumeweza na Tunazidi kusonga mbe/e: Akhasanteni kwa kunisikiliza.