SLIDE SHOWS ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA WAIGIZAJI MKOA WA KINONDONI......LOL

Chama Cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni Photos Slideshow: CHAMA’s trip to Dar es Salaam, Tanzania was created by TripAdvisor. See another Dar es Salaam slideshow. Take your travel photos and make a slideshow for free.

Thursday, January 17, 2013

MKUTANO WA WADAU WA FILAMU WAFANYA MAAMUZI MAZITO LEO VIJANA HOSTEL KINONDONI

HABARI WADAU ?

ULE MKUTANO MKUBWA SANA WA WADAU WA FILAMU ULIOTAJWA KUFANYIKA LEO PALE VIJANA HOSTEL KINONDONI,UMEMALIZIKA HIVI PUNDE.

LENGO.

1) LILIKUWA KUJADILI HATARI ILIYOPO MBELE YAO KTK SEKTA YA FILAMU ENDAPO KATIBU WA BODI YA FILAMU BIBI JOYCE FISOO ATAACHWA AENDELEE NA UTARATIBU WAKE WA KUPANGA MAMBO YANAYOIHUSU SEKTA YA FILAMU BILA KUSHIRIKISHA WANAFILAMU

2) HALI INAVYOENDELEA SASA YA KUINGIZA UTARATIBU WA KODI NA MALIPO YA HATUA MBALIMBALI ZA UTENGENEZAJI FILAMU BILA KUJALI HALI HALISI ILIVYO KTK SEKTA YA FILAMU

3) UPANGAJI WA UTARATIBU ZA KIKAZI NDANI YA SEKTA YA FILAMU BILA KUZINGATIA MASLAHI YA WATENDAJI WA SEKTA YA FILAMU KAMA MAHITAJI YA SOKO NA UTARATIBU WA MIKATABA ULIOPO SASA KUTOKANA NA UBOVU WA SOKO

4) UDHAIFU MKUBWA ULIOPO KTK TAASISI YA KUSIMAMIA HAKI MILIKI NA HAKI SHIRIKI (COSOTA) INAYOONGOZWA NA NDG. MKINGA

MAKUBALIANO YALIKUWA NI :

1) KUWAKATAA KWA PAMOJA NA KUONDOLEWA KTK TAASISI HUSIKA NDG.MKINGA WA( COSOTA) NA BIBI JOYCE FISOO WA BODI YA FILAMU.

2 )KUKUTANA KWA MARA YA PILI PALE PALE VIJANA KESHO SAA 4:00 ASUBUHI KWA LENGO LA KUKUSANYA NGUVU ZAIDI ILI KUKABILIANA NA TATIZO HILO LINALOBASHIRIWA KUANGAMIZA SEKTA YA FILAMU

3) KUITAKA SERIKALI KUIREJESHA (COSOTA )MIKONONI MWA WADAU KAMA LILIVYO LENGO LA UUNNDWAJI WAKE

4) KUIOMBA SERIKALI KUIVUNJA BODI YA FILAMU NA KUUNDA BODI YA FILAMU INAYOTOKANA NA WANA FILAMU KWA KUWA WANANAOIUNDA SASA WENGI WAO SI WANA FILAMU NA HAWAJUI ADHA ZILIZOPO KTK SEKTA YA FILAMU , HAWAKO TAYARI KUSHIRIKIANA NA WANA FILAMU KWA KISINGIZIO CHA KUWAITA HAWAKUSOMA JAMBO AMBALO SI LA KWELI, BADALA YAKE ITEUE MIONGONI MWA WANAFILAMU AMBAO BAADHI YAO WAMO WASOMI WAZURI WAFANYE KAZI ZA BODI HIYO

5) KUZIKATAA KWA NGUVU ZOTE KANUNI ZA BODI YA FILAMU ZILIZOTOKA MWAKA JANA KWA KUWA HAZINA USHIRIKI WAO NA HAZIKUZINGATIA HALI HALISI YA SEKTA YA FILAMU KWA TANZANIA

Wednesday, January 16, 2013

MKUTANO MKUBWA SANA WA WADAU WOTE WA FILAMU

waigizaji wa FILAMU na WADAU WOTE wa FILAMU wanahitajika kwa wingi kufika kesho kuanzia saa 4:00 asubuhi ktk ukumbi wa VIJANA HOSTEL KINONDONI ili kuinusuru sekta ya filamu kutoka katika mpango wa kidhalimu unaoratibiwa na baadhi ya watendaji wa serikali kama katibu wa BODI ya FILAMU bibi JOYCE FISOO na MKURUGENZI wa COSOTA ndg.MKINGA,hawa wote kwa pamoja wamegundulika kuwa ndio waratibu wa UMASIKINI wa WASANII wa FILAMU na MUZIKI wa TANZANIA


HALA HALA  ILI KUONDOKANA NA UMASIKINI ULIOKITHIRI KWA WASANII WALIO WENGI WA FILAMU TUFIKE ILI TUAMUE HATMA YA MAISHA YETU NA VIZAZI VYETU,   

   MKATAE  NDG. MKINGA ,MKATAE   BIBI    JOYCE FISOO KWA  MAENDELEO YA FILAMU NA TASNIA KWA UJUMLA WAKE.
RAIS wa shirikisho la FILAMU Tanzania MH.Simon Mwakifwamba akiwa na bodi yake ya shirikisho la filamu wakizungumza na wasanii wa filamu na viongozi wa vyama wanachama wa shirikisho la FILAMU mbele yao ( hawapo pichani ) ktk mkutano mkubwa wa wadau wa FILAMU kuhusiana na salamu za mkuu wa nchi MH. DR. JAKAYA KIKWETE alizowapa  walipozungumza wakati wa maziko ya marehemu JUMA KILOWOKO (SAJUKI) mwanzoni mwa mwezi wa kwanza mwaka 2013