SLIDE SHOWS ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA WAIGIZAJI MKOA WA KINONDONI......LOL

Chama Cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni Photos Slideshow: CHAMA’s trip to Dar es Salaam, Tanzania was created by TripAdvisor. See another Dar es Salaam slideshow. Take your travel photos and make a slideshow for free.

Thursday, January 17, 2013

MKUTANO WA WADAU WA FILAMU WAFANYA MAAMUZI MAZITO LEO VIJANA HOSTEL KINONDONI

HABARI WADAU ?

ULE MKUTANO MKUBWA SANA WA WADAU WA FILAMU ULIOTAJWA KUFANYIKA LEO PALE VIJANA HOSTEL KINONDONI,UMEMALIZIKA HIVI PUNDE.

LENGO.

1) LILIKUWA KUJADILI HATARI ILIYOPO MBELE YAO KTK SEKTA YA FILAMU ENDAPO KATIBU WA BODI YA FILAMU BIBI JOYCE FISOO ATAACHWA AENDELEE NA UTARATIBU WAKE WA KUPANGA MAMBO YANAYOIHUSU SEKTA YA FILAMU BILA KUSHIRIKISHA WANAFILAMU

2) HALI INAVYOENDELEA SASA YA KUINGIZA UTARATIBU WA KODI NA MALIPO YA HATUA MBALIMBALI ZA UTENGENEZAJI FILAMU BILA KUJALI HALI HALISI ILIVYO KTK SEKTA YA FILAMU

3) UPANGAJI WA UTARATIBU ZA KIKAZI NDANI YA SEKTA YA FILAMU BILA KUZINGATIA MASLAHI YA WATENDAJI WA SEKTA YA FILAMU KAMA MAHITAJI YA SOKO NA UTARATIBU WA MIKATABA ULIOPO SASA KUTOKANA NA UBOVU WA SOKO

4) UDHAIFU MKUBWA ULIOPO KTK TAASISI YA KUSIMAMIA HAKI MILIKI NA HAKI SHIRIKI (COSOTA) INAYOONGOZWA NA NDG. MKINGA

MAKUBALIANO YALIKUWA NI :

1) KUWAKATAA KWA PAMOJA NA KUONDOLEWA KTK TAASISI HUSIKA NDG.MKINGA WA( COSOTA) NA BIBI JOYCE FISOO WA BODI YA FILAMU.

2 )KUKUTANA KWA MARA YA PILI PALE PALE VIJANA KESHO SAA 4:00 ASUBUHI KWA LENGO LA KUKUSANYA NGUVU ZAIDI ILI KUKABILIANA NA TATIZO HILO LINALOBASHIRIWA KUANGAMIZA SEKTA YA FILAMU

3) KUITAKA SERIKALI KUIREJESHA (COSOTA )MIKONONI MWA WADAU KAMA LILIVYO LENGO LA UUNNDWAJI WAKE

4) KUIOMBA SERIKALI KUIVUNJA BODI YA FILAMU NA KUUNDA BODI YA FILAMU INAYOTOKANA NA WANA FILAMU KWA KUWA WANANAOIUNDA SASA WENGI WAO SI WANA FILAMU NA HAWAJUI ADHA ZILIZOPO KTK SEKTA YA FILAMU , HAWAKO TAYARI KUSHIRIKIANA NA WANA FILAMU KWA KISINGIZIO CHA KUWAITA HAWAKUSOMA JAMBO AMBALO SI LA KWELI, BADALA YAKE ITEUE MIONGONI MWA WANAFILAMU AMBAO BAADHI YAO WAMO WASOMI WAZURI WAFANYE KAZI ZA BODI HIYO

5) KUZIKATAA KWA NGUVU ZOTE KANUNI ZA BODI YA FILAMU ZILIZOTOKA MWAKA JANA KWA KUWA HAZINA USHIRIKI WAO NA HAZIKUZINGATIA HALI HALISI YA SEKTA YA FILAMU KWA TANZANIA

Wednesday, January 16, 2013

MKUTANO MKUBWA SANA WA WADAU WOTE WA FILAMU

waigizaji wa FILAMU na WADAU WOTE wa FILAMU wanahitajika kwa wingi kufika kesho kuanzia saa 4:00 asubuhi ktk ukumbi wa VIJANA HOSTEL KINONDONI ili kuinusuru sekta ya filamu kutoka katika mpango wa kidhalimu unaoratibiwa na baadhi ya watendaji wa serikali kama katibu wa BODI ya FILAMU bibi JOYCE FISOO na MKURUGENZI wa COSOTA ndg.MKINGA,hawa wote kwa pamoja wamegundulika kuwa ndio waratibu wa UMASIKINI wa WASANII wa FILAMU na MUZIKI wa TANZANIA


HALA HALA  ILI KUONDOKANA NA UMASIKINI ULIOKITHIRI KWA WASANII WALIO WENGI WA FILAMU TUFIKE ILI TUAMUE HATMA YA MAISHA YETU NA VIZAZI VYETU,   

   MKATAE  NDG. MKINGA ,MKATAE   BIBI    JOYCE FISOO KWA  MAENDELEO YA FILAMU NA TASNIA KWA UJUMLA WAKE.
RAIS wa shirikisho la FILAMU Tanzania MH.Simon Mwakifwamba akiwa na bodi yake ya shirikisho la filamu wakizungumza na wasanii wa filamu na viongozi wa vyama wanachama wa shirikisho la FILAMU mbele yao ( hawapo pichani ) ktk mkutano mkubwa wa wadau wa FILAMU kuhusiana na salamu za mkuu wa nchi MH. DR. JAKAYA KIKWETE alizowapa  walipozungumza wakati wa maziko ya marehemu JUMA KILOWOKO (SAJUKI) mwanzoni mwa mwezi wa kwanza mwaka 2013

Friday, December 14, 2012

TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA KIKATIBA.

YAH:MKUTANO MKUU WA KIKATIBA WA CHAMA CHA WAIGIZAJI KINONDONI UTAKAOFANYIKA J,MOSI  TAR. 22/DECEMBER/2012  KUANZIA SAA 4:00  ASUBUHI UKUMBI PALE PALE VIJANA HOSTEL KINONDONI.WANACHAMA WOTE MNATAKIWA KUHUDURIA BILA KUKOSA NI MUHIMU SANA KWA USTAWI WA CHAMA..AMKA TAFF NURU YA HAKI..BY MAKAM M/KITI  SALUM HUSSEIN CHILWA.

TAARIFA RASMI KWA WAIGIZAJI WOTE.



waigizaji wote wanatakiwa kuwa ndani ya mfumo rasmi unaotambulika ktk sekta ya filamu kuanzia tarehe 1/january/2013.Na  kila mdau wa taaluma inayohusiana na filamu anatakiwa awe amejisajili ktk chama kinachohusiana na taaluma yake vinginevyo hataruhusiwa kufanya kazi yoyote inayo husiana na filamu kuanzia tarehe hiyo.Hivyo basi TDFAA mkoa wa kikatiba kinondoni inawahimiza wale wote wenye mapenzi mema na sekta ya filamu Tanzania kuitumia fursa hii kwa wakati ili kuepuka usumbufu wowote unaoweza kuwapata kutokana na utekelezaji wa mpango huu wa serikali kuifanya sekta ya filamu kuwa rasmi kuanzia tar.1/january/2013 tunawatakia ujenzi mwema wa taifa la TANZANIA na SEKTA ya FILAMU,PAMOJA TUNAWEZA. AMKA TAFF NURU YA HAKI

Friday, April 6, 2012

RAIS WA SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIZ APATA MSIBA MKUBWA....

RAIS WA SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA AMEPATA MSIBA MKUBWA USIKU WA KUAMKIA JANA WA KUFARIKI KWA MTOTO WAKE WA KIUME BENJAMIN SAIMON MWAKIFAMBA AMBAE ALIKUWA ANASUMBULIWA NA LIMONIA KWA SIKU MBILI HUKO MBEYA NA KUFARIKI DUNIA 13 MAR 2012 TUNAMUOMBEA MWENYEZI MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI PAMOJA NA KUIPA NGUVU FAMILIA KWA UJUMLA KATIKA WAKATI HUU MGUMU AMIN.....

Sunday, February 19, 2012

SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA LAFANYA SEMINA YA VIONGOZI WA VYAMA...

 Mh rais wa shirikisho la filamu tanzania akiwa na makamu wake na katibu wake na mwongozaji wa semina ya viongozi wa vyama vyote uliofanyika basata.......17 feb 2012
 viongozi wa vyama wakiwa makini...
 mh mwenyekiti mkoa wa kinondoni na mwenyekiti wa temeke wkimsikiliza muongozaji wa semina iliofanyika basata...
Muongozaji wa semina ya viongozi wa vyama vyote vinavyounda shirikisho la filamu tanzania...TAFF