SLIDE SHOWS ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA WAIGIZAJI MKOA WA KINONDONI......LOL

Chama Cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni Photos Slideshow: CHAMA’s trip to Dar es Salaam, Tanzania was created by TripAdvisor. See another Dar es Salaam slideshow. Take your travel photos and make a slideshow for free.

Friday, December 14, 2012

TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA KIKATIBA.

YAH:MKUTANO MKUU WA KIKATIBA WA CHAMA CHA WAIGIZAJI KINONDONI UTAKAOFANYIKA J,MOSI  TAR. 22/DECEMBER/2012  KUANZIA SAA 4:00  ASUBUHI UKUMBI PALE PALE VIJANA HOSTEL KINONDONI.WANACHAMA WOTE MNATAKIWA KUHUDURIA BILA KUKOSA NI MUHIMU SANA KWA USTAWI WA CHAMA..AMKA TAFF NURU YA HAKI..BY MAKAM M/KITI  SALUM HUSSEIN CHILWA.

TAARIFA RASMI KWA WAIGIZAJI WOTE.



waigizaji wote wanatakiwa kuwa ndani ya mfumo rasmi unaotambulika ktk sekta ya filamu kuanzia tarehe 1/january/2013.Na  kila mdau wa taaluma inayohusiana na filamu anatakiwa awe amejisajili ktk chama kinachohusiana na taaluma yake vinginevyo hataruhusiwa kufanya kazi yoyote inayo husiana na filamu kuanzia tarehe hiyo.Hivyo basi TDFAA mkoa wa kikatiba kinondoni inawahimiza wale wote wenye mapenzi mema na sekta ya filamu Tanzania kuitumia fursa hii kwa wakati ili kuepuka usumbufu wowote unaoweza kuwapata kutokana na utekelezaji wa mpango huu wa serikali kuifanya sekta ya filamu kuwa rasmi kuanzia tar.1/january/2013 tunawatakia ujenzi mwema wa taifa la TANZANIA na SEKTA ya FILAMU,PAMOJA TUNAWEZA. AMKA TAFF NURU YA HAKI

Friday, April 6, 2012

RAIS WA SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIZ APATA MSIBA MKUBWA....

RAIS WA SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA AMEPATA MSIBA MKUBWA USIKU WA KUAMKIA JANA WA KUFARIKI KWA MTOTO WAKE WA KIUME BENJAMIN SAIMON MWAKIFAMBA AMBAE ALIKUWA ANASUMBULIWA NA LIMONIA KWA SIKU MBILI HUKO MBEYA NA KUFARIKI DUNIA 13 MAR 2012 TUNAMUOMBEA MWENYEZI MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI PAMOJA NA KUIPA NGUVU FAMILIA KWA UJUMLA KATIKA WAKATI HUU MGUMU AMIN.....

Sunday, February 19, 2012

SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA LAFANYA SEMINA YA VIONGOZI WA VYAMA...

 Mh rais wa shirikisho la filamu tanzania akiwa na makamu wake na katibu wake na mwongozaji wa semina ya viongozi wa vyama vyote uliofanyika basata.......17 feb 2012
 viongozi wa vyama wakiwa makini...
 mh mwenyekiti mkoa wa kinondoni na mwenyekiti wa temeke wkimsikiliza muongozaji wa semina iliofanyika basata...
Muongozaji wa semina ya viongozi wa vyama vyote vinavyounda shirikisho la filamu tanzania...TAFF

MKUTANO MKUBWA WA CHAMA CHA WASAMBAZAJI WAFANA SANA BASATA...

 Picha ya pamoja ya wasambazaji wa kazi za wasanii baada ya mkutano basata..13 feb 2012
 Mh rais wa shirikisho la filamu tanzania saimon mwakifamba akiwaongoza wasambazaji wa filamu wakiwepo na steps ent:....
 Ndugu jay na kambarage wa steps ent: wakimsikiliza rais wa shirikisho la filamu tanzania Mh saimon mwakifamba....steps ni mmoja wa wanachama wa shirikisho hilo TAFF.
 Mh shuu mjumbe wa chama cha wasambazaji akiwa makini kuskiliza maoni ya wasambazaji pia kwenye mkutano uliofanyika dar...
wanachama wa chama cha wasambasaji wakipanga mikakati yao ya jinsi gani wa kuwadhibiti maharamia wa kazi za wasanii.....

Saturday, January 21, 2012

NATASHA NDANI YA 100.5 TIMES FM J.PILI 22 JAN 2012


TANGAZO:.... MTANGAZAJI MAARUFU TANZANIA NATASHA KESHO SIKU YA J.PILI 22 JAN 2012 NDIO SIKU YAKE YA KWANZA KURUSHA KIPINDI CHA RADIO KINACHOZUNGUMZIA TASNIA YA FILAMU TANZANIA RADIO TIMES 100.5 FM STRERIO  KUANZIA SAA 5 ASUBUHI MPAKA SAA 6 MCHANA AKISHIRIKIANA NA MONALISA USIKOSE UHONDO HUO NA KUCHANGIA PIA MSIKILIZAJI KUCHAGUA JINA LA KIPINDI HICHO.....AMKAA TAFF NURU YA HAKI....

MKUTANO MKUBWA KUCHAMBUA KANUNI ZA BODI YA FILAMU TANZANIA 16 JAN 2012

 Umati wa wasanii waliofurika katika ukumbi wa vijana kinondoni kujadili kanuni za bodi ya filamu tanzania
 Katibu mkuu wa shirikisho la filamu tanzania ndugu wilson makubi akitoa maelezo ya awali kabla ya kikao kuanza..
 Steven kanumba akichangia mawazo yake na kusema kanuni za bodi ya filamu ni hazifai inabidi zibadilishwe zote kwa kushirikiana na wasnii na sio wao peke yao...
 Jacob stevene akiwa nae mmoja wapo aliekuwepo katika mkutano huo..
 Chiki mchomi akitoa mawazo yake pia na kusema kuwa kanuni za bodi ya filamu hazifai na cha msingi zifutwe zotee...
 William mtitu akitoa mawazo yake na kuonekana anapotosha umma baada ya kusema taff haiusiki katika kusimamia mkutano huo kwa maana taff haikuainishwa ndani ya kanuni hizo...

 Steve nyerere nae alichangia vizuri sana katika mkutano huo....
 Rich akiwa makini nae kumsikiliza mwenyekiti wa chama cha waigizaji taifa mike sangu...
wasanii mbali mbali walikuwepo kuchangia kanuni hizo na hitimisho wa mkutano huo ni kwamba   WASANII KWA PAMOJA HATUKUBALIANI NA KANUNI YA BODI YA FILAMU TANZANIA NA ZIFUTWE ZOTE HAZIFAI HATA KIDOGO CHA MSINGI TUKAE KWA PAMOJA NA WASANII TUCHANGIE MAMBO YETU YANAYOTUHUSU..MAANA HIZO KANUNI ZINATUKANDAMIZA WASANII NA KUUA TASNIA NZIMA YA FILAMU TANZANIA ...HATUZITAKIIIII.....

Wednesday, January 18, 2012

MYAMBA AFUNGUA CHUO CHA FILAMU (TFTC)

 Wanafunzi wa chuo cha tasnia ya filamu wakiwa makini kuskiliza uongozi na wageni wa heshima wakifungua rasmi chuo hicho 9 jan 2012 ubungo plaza dar-es-salaam...
 Rais wa shirikisho la filamu tanzania saimon mwakifamba na katibu wa shirikisho wilson makubi na mzee kitime na mkurugenzi wa chuo ndungu myamba...baada ya kufunguliwa rasmi chuo hicho....
 Mkurugenzi Emanuel myamba akitoa ufafanuzi juu ya taratibu zote za chuo...
 Waandishi wa habari walipokuwa pamoja na wanafunzi na viongozi wa chuo na wageni waalikwa katika uzinduzi huo wa chuo...9 jan 2012
 Mhasibu wa chuo cha TANZANIA FILM TRAINING CENTER(TFTC) MH Wilson makubi akitoa maelekezo ya awali ya chuoni...
Mwanafunzi akisoma hutuma kwa mgeni rasmi saimon mwakifamba kabla ya kukifungua rasmi...

Tuesday, January 17, 2012

20 DAZEN PARTY YA BAUCHA INC...14 JAN 2012

 Mwenyekiti wa chama cha waigizaji mkoa wa kinondoni ali baucha na katibu wake ndugu willson ishengoma wakiwa na wasanii bora wa kike na kiume wa mwaka katika kundi la baucha inc na tunzo zao...
 Wasanii wa kundi baucha inc katika picha ya pamoja 14 jan 2012
 Kaka mkuu akiwa na tunzo yake ya kuwa msanii bora wa kiume wa kundi mwaka 2011-2012 Kassim kondo....
 Kaka mkuu kassim na dada mkuu jovina wa baucha inc wakiwa na msanii bora wa kike wa 2011- 2012 wa kundi hilo therapia....
 Wasanii wakipata chakula cha usiku...
 Baucha inc..
wasanii wakipata chakula ndani ya party ya 20 dazen ya baucha inc...

MAZISHI YA MZEE FUNDI SAIDI(MZEE KIPARA)

 Mwenyekiti wa chama cha waigizaji mkoa wa kinondoni ali baucha wakiwa ndani ya gari walipokwenda kuuchukua mwili wa marehemu mzee kipara hospital ya mwananyamala kwa mazishi
 Mzee small alikuja na ubao wake mwenyewe kwa ajili ya kuzikiwa marehemu mzee kipara...
 Mh samwel sita waziri wa afrika mashariki akiongea machache kuhusiana na anavyomjua mzee kipara toka mh waziri alipokuwa tabora...
 Rais wa shirikisho la filamu tanzania akiwa na waziri wa afrika mashariki Mh samwel sita wakisikiliza kwa makini historia ya maisha ya marehemu mzee fundi saidi(kipara)
 waheshimiwa wakipata rizki kabla ya maziko...
 Mwenyekiti wa chama cha waigizaji mkoa wa kinondoni pamoja na mh mbunge wa kinondoni iddi azan na katibu mkuu wa chama cha waigizaji mkoa wa kinondoni wakibadilishana mawazo kuhusu msiba huo wa mzee wetu...
safari kuelekea makaburini...
mazishi....

 steven kanumba mmoja wa wasanii waliokuwepo kumzika marehemu mzee kipara...
 Jb..rich..shija nao walikuwepo nao
 Cheni na cloud nao walishiriki kikamilifu katika mazishi...
 Joti nae ndani...
 Masanja pia...

Wednesday, January 11, 2012

MZEE KIPARA AFARAIKI DUNIA


Msanii Mkongwe katika tasnia ya Maigizo/Filamu hapa nchini, Fundi Saidi almaarufu kwa jina la kisanii Mzee Kipara amefariki mapema leo asubuhi,nyumbani kwake huko Kigogo Mbuyuni-Kinondoni jijini dar.

Mzee kipara ambaye alizaliwa mnamo mwaka 1922,huko Bongoni mkoani Tabora,alikuwa kisumbuliwa na matatizo ya miguu kukosa nguvu,alikuwa hawezi kusimama  mwenyewe,sambamba na umri nao huenda ulichangia kwa maradhi hayo na mengineyo,hali iliyokuwa ikimlazimu kutumia muda  mwingi kitandani,wakati mwingine alishindwa kutoka nje mpaka watu watokee kumtoa nje ili kuota jua ama kupunga upepo.

Mzeee Kipara alianza sanaa  mnamo mwaka 1964 kwa kufanya kazi za mitaani na baadaye akachukuliwa na Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) sasa TBC Taifa. Akiwa na kituo hicho, aliigiza katika michezo mingi na nafasi zake kubwa zilikuwa zile zenye kuonesha utemi, wengi huita ukorofi. Mnamo Mwaka 1999, akiwa na wasanii wenzake akina Zena Dilip, Rasia Makuka, marehemu Rajab Hatia  ‘Mzee Pwagu’ na Mama Haambiliki walijiunga katika Kundi la Kaole ambalo lilikuwa likirusha maigizo yake katika Runinga ya ITV.

Taarifa zaidi za msiba huo na mazishi tutafahamishana zaidi hapo baadaye kidogo.MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI -AMIN.

Thursday, January 5, 2012

CHAMA CHA WAIGIZAJI CHAENEZA KANUNI ZA BODI YA FILAMU TANZANIA..

  Mtangazaji wa redio uhuru natasha akiwahoji viongozi wa chama cha uigizaji mkoa wa kinondoni..
 makamu mwenyekiti wa chama cha waigizaji mkoa wa kinondoni salum chilwa na katibu wake wilson ishengoma wakielezea kwa undani kanuni za bodi ya filamu tanzania...
 Mh chilwa na Mh wilson wakijibu masali kutoka kwa wasikilizaji leo 5 jan 2012 radio uhuru..