SLIDE SHOWS ZA WANACHAMA WA CHAMA CHA WAIGIZAJI MKOA WA KINONDONI......LOL

Chama Cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni Photos Slideshow: CHAMA’s trip to Dar es Salaam, Tanzania was created by TripAdvisor. See another Dar es Salaam slideshow. Take your travel photos and make a slideshow for free.

Monday, December 19, 2011

UCHAGUZI WA TAFF WAKARIBIA TAREHE 22 DEC 2011..

NDUGU SAIMON MWAKIFAMBA.


WANACHAMA WA SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA...WOTE MNAOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI SIKU YA UCHAGUZI TAREHE 22 DEC 2011 BASATA ILALA DAR-ES-SALAAM SAA NNE ASUBUHI KUSHUHUDIA KUPATIKANA KWA VIONGOZI WA KWANZA KIKATIBA WA SHIRIKISHO HILO TOKA LIUNDWE, USIKOSE KUJUA VIONGOZI WAKOOOO.....AMKA..NURU YA HAKI....

SAFARI ZA KUTEMBELEA VIKUNDI ZAENDELEA (KIBAFUTE,NEW VISION ARTS...)

 new vision arts group wakiwa na viongozi wa chama cha waigizaji mkoa wa kinondoni...
 kibafute group wakiwa pamoja na viongozi pia...
 mwalimu wa new vision arts ndugu  nwaka...


 msanii wa new vision bi sura akiuliza swali pia...
mkurugenzi wa new vision arts  ndugu okasha akiuliza swali kwa viongozi..

Thursday, December 15, 2011

MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAIGIZAJI MKOA WA PWANI AFIWA NA MZAZI WAKE..

 Waumini wakiusalia mwili wa marehemu mohammed simba aliefariki jana tarehe 14 dec 2011 saa sita mchana huko kibaha ..mwenyezi mungu ailaze roho yake mahali pema peponi...amin
 mwili wa marehemu mzee mohamed simba ukiteremshwa ndani ya kaburi kongowe mkoa wa pwani...
 Rais wa shirikisho la filamu tanzania (TAFF)Saimon mwakifamba akiwa na viongozi mbalimbali wa vyama alipokuwa pamoja na kiongozi mwenzao wa pwani aliefiwa na mzazi wake kabla ya mazishi nyumbani kwa marehemu mzee Mohamed simba ambae ni baba wa mwenyekiti wa chama cha wigizaji mkoa wa pwani...
 mwenyekiti wa chama cha waigizaji mkoa wa pwani Mh simba.m. simba..
viongozi mbali mbali wa ccm na vyama vingine nao walijumuika katika mazishi hayo yaliofanyika kongowe,kibaha...

Saturday, December 10, 2011

MATUKIO MBALIMBALI YA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA

Rais Jakaya Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania kikosi hiki ni cha Jeshi la Wananchi wanawake

Rais Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na viongozi wa nchi mbalimbali waliohudhuria katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania yanayofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam mchana huu hapa akisalimiana na Rais wa Namibia Mheshimiwa Hifikepunye Pohamba.

Rais jakaya Kikwete akipokea heshima wakati mizinga ikipigwa na jeshi la wananchi kwa heshima ya Rais.

Rais Dk. Jakaya Kikwete akipungia mkono wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja wa uhuru kwa ajili ya kuongoza sherehe za miaka 50 ya Tanzania.
Msafara wa Rais Dk Jakaya Kikwete ukiwasili kwenye uwanja wa Uhuru tayari kwa kuongoza watanzania katika sherehe za miaka 50 ya Tanzania.

Thursday, December 8, 2011

SHERIA NA KANUNI ZA TASNIA YA FILAMU TANZANIA..


HOTUBA YA MGENI RASMI - KAIMU KATIBU MKUU BIBI SIHABA NKINGA KATIKA UFUNGUZI WA KIKAO CHA WADAU WA FILAMU KUHUSU MJADALA WA MUSTAKABALI WA TASNIA YA FILAMU KATIKA KUSHEREKEA MIAKA 50 YA UHURU NA NINI MKAKATI KATIKA MIAKA 50 IJAYO. TAREHE 07/11/2011- KATIKA UKUMBI WA VIJANA SOCIAL- KINONDONI
Ndugu viongozi na Watendaji wa Wizara
Ndugu viongozi na watendaji wa Bodi ya Filamu
Ndugu viongozi wa Shirikisho la Filamu na wanachama
Ndugu wadau wa filamu
Ndugu wanahabari
Mabibi na mabwana
Awali ya yote napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kutupa uhai na kutuwezesha kukutana hapa.  Aidha natoa shukrani nyingi kwa kunialika kuwa mgeni katika mjadala huu muhimu ukiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru. Wizara yetu imefarijika sana na jambo hili.
Ndugu washiriki,
Katika mjadala huu nimeelezwa kuwa mtapata fursa ya kuona filamu za zamani na kupitishwa katika mada tatu ambazo ni :- Hali ya Tasnia ya Filamu kabla ya uhuru mpaka sasa, Nini wajibu wa wadau wa filamu katika mstakabali wa kukua kwa tasnia ya filamu nchini na Mapitio ya Sheria na Kanuni za Filamu
Ndugu washiriki,
Ni imani yangu mtajadili kwa kina kuhusu tasnia ya filamu na mtafikia mahali pa kupata dira ya nini tufanye katika miaka 50 ijayo. Aidha ninasihi katika majadiliano yenu mzingatie namna ya kuondokana na changamoto kadhaa ambazo zimekuwa kero kwa jamii. Changamoto hizo ni pamoja na :-
·         Uwepo wa filamu nyingi zisizo na maadili,
·         ukiukwaji wa Sheria ikiwemo wakati wa utengenezaji, uonyeshwaji, usambazaji
       •      uingizaji holela wa filamu za nje na wasanii;
kuibuka kwa utitiri wa vibanda visivyo rasmi vinavyoonyesha filamu/video,
·         uharamia wa kazi za wasanii wa filamu.
·         filamu nyingi zinazotengenezwa kukosa weledi na kutoendana na utamaduni wa nchi, kutotangaza Utaifa, mandhari na fursa zilizopo kwa utambulisho wa taifa letu na lugha yetu ya Kiswahili na
·         wafanyakazi katika tasnia ya filamu kutopata mapato stahiki yatokanayo na jasho lao na pia Serikali kutopata maduhuli stahili yatokanayo na filamu.

Ndugu washiriki,
Mambo niliyotaja juu yapo ndani ya uwezo wenu kwani miongoni mwenu wapo watayarishaji, wasambazaji, waingizaji filamu kutoka nje, waandishi wa miswada waonyeshaji, waendeshaji wa maeneo ya maonyesho, waongozaji na waigizaji nk. Ni
matarajio ya Seriakali kwamba kila mmoja akijitambua na kutimiza wajibu wake tutaondokana na changamoto nilizozitaja juu. Aidha ninawasihi sana kufuata Taratibu, Kanuni, na Sheria nina hakika Mwanasheria wetu wa Wizara atawapitisha kwa kina.

Ndugu washiriki,
Katika nchi za wenzetu tasnia ya filamu inatoa ajira na pate kubwa kwa wasanii na pia katika uchumi wa nchi, hali ni tofauti hapa kwetu, umefika wakati sasa kwa wasanii kutoendelea kuwa na hali duni na watu wachache kufaidi jasho lao. Ongezeni ushirikiano na imarisheni umoja miongoni mwenu. Ninatambua kuwa mna vyama tisa na vyama hivyo ni wanachama wa Shirikisho la Filamu. Nia ya Serikali katika kuruhusu uanzishwaji wa vyombo hivyo ni ili kuwe na kiungo kati yenu na Serikali. Na Serikali kupitia wizara yetu imekuwa ikiwapa ushirikiano wa hali ya juu. Sina mashaka pia nao watapata fursa ya kuzungumzia umuhimu wa umoja wenu katika kusherekea miaka 50 ya Uhuru.
Ndugu washiriki,
Katika malengo ya miaka 50 ijayo; Ni matumaini ya wizara kwamba mtatengeneza filamu zenye ubunifu wa hali ya juu, weledi na viwango bila kuathiri maadili na utamaduni wetu ; ili ziweze kuingia katika soko la ushindani. Aidha hakikisheni filamu zenu zinapitia katika mamlaka inayosimamia tasnia ya filamu kabla ya utengenezaji, usambazaji, uuzaji na uonyeshaji kama sheria inavyotutaka. Kwa wale wanoapeleka filamu nje au kushiriki katika matamsha mbalimbali ijulisheni Wizara ili mpate baraka za kuipeperusha bendera yetu kwani huko mnakwenda kuitangaza nchi.
Mwisho natoa rai kwa wale wote ambao filamu zao bade hazijasilishwa kwa ukaguzi wala miswada yao kupitishwa na Bodi ya Filamu wakumbuke muda waliopewa na Serikali wa kuwasilisha kwa hiari ni miezi mitatu kuanzia tarehe 13/10/2011. Kwa kuwa walengwa ni ninyi natumia fursa hii kuwakumbusheni.
Nawatakia mjadala mwema ni mani yangu utakuwa na tija kwa tasnia ya filamu na Taifa kwa ujumla.
Tumethubutu, Tumeweza na Tunazidi kusonga mbe/e: Akhasanteni kwa kunisikiliza.

Wednesday, December 7, 2011

SERIKALI YATOA SHERIA NA KANUNI ZAKE ZA TASNIA YA FILAMU TANZANIA..

mkurugenzi wa utamaduni mr mwansoko akisoma hutuba yake leo kwa wadau,wanachama na wapenzi wa tasnia ya filamu tanzania kwenye mkutano mkubwa uliofanyika mjini dar-es-salam.. 

katibu wa bodi ya filamu tanzania mrs Joice.g. Fissoo akisoma kanuni kwa wadau wanachama  kuwa kabla tarehe 13 jan 2012 film zote za nje na ndani zijisalimishe kwa hiyari bodi ya filamu kwa ukaguzi na kuanza kutumika kwa sheria hizo na kanuni zake...

MKUTANO MKUBWA WA WADAU WA TASNIA YA FILAMU TANZANIA WAFANA SANA..

mkurugenzi wa idara ya utamaduni prof: mwansoko akiwa na viongozi wa vyama mbali mbali vya tasnia ya filamu tanzania kabla ya mkutano wa kushereke miaka 50 ya uhuru wa tanzania na mustakabali mzima wa miaka 50 ijayo ya tasnia ya filamu tanzania uliofanyika leo 7 dec 2011..ukumbi wa vijana kinondoni...
Prof: mwansoko akisoma hutuba yake
mrs joice.g. fisoo akizifafanua sheria na kanuni za tasnia ya filamu tanzania
wakili wa bodi ya filamu tanzania ndugu kipangule akielezea pia kanuni kisheria zaidi...
rais wa shirikisho la filamu tanzania saimoni mwakifamba akisisitiza wadau na wasanii kujiunga na vyama vyao haraka sana kabla ya tarehe 13 jan 2012..kuwa ni muhimu sana kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla..
umati wa wasanii na wadau wa tasnia ya filamu tanzania ulivyofurika leo.....kazi imeanza sasa...
mwenyekiti wa chama cha waigizaji taifa mike sangu
john lister akiuliza swali kwa wakili wa bodi ya filamu tanzani..
viongozi wa serikali wakiwa na viongozi mbalimbali...kabla ya mkutano..
mwenyekiti wa jumuia ya waandaaji na wacheza filamu  kutoka visiwa vya zanzibar ndugu msellemu issa musellem..
viongozi wa serikali wakipiga picha na viongozi wa vyama na vikundi vya tasnia ya filamu tanzania.
deo songa akiwa na patna wake...
msanii mtanga na katibu wa chama cha waigizaji mkoa wa kinondoni wilson ishengoma

mwenyekiti wa chama cha waigizaji mkoa wa temeke ndugu dille akiwa na mjumbe wa kamati ya fedha,uchumi na mipango wa kinondoni ndugu doller enock na bi mwenda wakifatilia kwa makini kujua kanuni zilizotolewa jana...
mnyamba akiuliza swali la kanuni inayosema kuwa kuanzia januari nilazima ulipie laki tano (500,000)ili upate kibali cha kufanya filamu...
Mzee katembo nae akimsikiliza mwanasheria wa bodi ya filamu tanzania ndugu kipangule alipokuwa akizitaja sheria na kanuni leo vijana kinondoni...